Saturday, February 26, 2011
Maunda Zoro kumiliki Bendi Tanzania
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Maunda Zoro asema hivi karibuni ataanzisha Bendi yake mwenyewe. Akizungumza na Mwananchi Jumapili hivi karibuni, Maunda alisema; “Wazo la kuanzisha bendi nilipewa na kaka (Banana Zoro), lakini taratibu za kuanzisha bendi hiyo bado kidogo kukamilika. Alisema kuna baadhi ya vifaa havijakamilika, lakini anategemea hadi Aprili mwaka huu atakuwa tayari ameshaianzisha ikiwamo kusajili bendi hiyo. “Jina la bendi bado sijalifikiria, ingawa nitawashirikisha baadhi ya wanamuziki wa Bongo fleva ambao sitawataja majina kwa sasa, kwani ni mapema mno,” alisema Maunda. Maunda alitamba na wimbo wa ‘Niwe wako’ na ‘Mapenzi ni ya wawili’ na ameshirikishwa kwenye nyimbo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hellow wa Hussein Machozi na ‘Usinihukumu’ wa Steve.