Training and Event

Action Music Tanzania (AMTZ) yenye namba ya usajili bst/4733 itatoa mafunzo ya upigaji wa ala mbalimbali za muziki (kwa vitendo) kwa watu wote
Mafunzo yataanza: Tarehe 16/07/2012

Mahali: Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) Chuo Kikuu cha Dar es salaam (sehemu ya Mlimani)

Njoo ujifunze mbinu za kitaalamu za kupiga/kucheza  gitaa, keyboard/piano, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili ya tanzania, bila kusahau mafunzo maalumu ya “body percussion” (matumizi ya mwili kutengeneza midundo ya muziki) na usomaji wa “notation” yatakaotolewa na wataalam waliobobea katika tasnia ya muziki kutoka vyuo mbalimbali.

Usajili unafanyika: Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Mlimani)

Fomu za usajili zinapatikana FPA kila siku kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa gharama ya shilingi 3000/= tu. wahi, nafasi ni chache.

Gharama za mafunzo
Kila mshiriki katika mafunzo haya atalipia gharama ya sh.50,000 kwa mwezi ikiwa ni swan a sh.150,000 kwa kipindi cha miezi mitatu. malipo yanatakiwa kulipwa kabla ya mshirki kuanza mafunzo kupitia namba ya akaunti ya benki ya CRDB, Action Music Tanzania, 0150395755200 na kwenda na nakala ya malipo hayo wakati wa mafunzo au kwenda kulipa moja kwa moja chuoni.

Ratiba ya mafunzo
Mafunzo yatafanyika siku za jumatano, jumamosi na jumapili kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, kwa wafanyakazi wanaopenda kusoma jioni tuu, mafunzo yatatolewa kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni.

Vitendea kazi
AMTZ itatoa vifaa vya muziki kwa kila mshiriki lakini unashauriwa kuja na chombo chako ili kuboresha mazingira ya kujifunza,AMTZ itatoa nakala ya masomo yanayofundishwa na wanafunzi watatakiwa kutoa nakala za notisi hizo.


0 comments:

Post a Comment