Msanii
wa Hip Hop, Joseph Haule aka Professor J jana amekitembelea chama cha
haki miliki Tanzania, ‘COSOTA’ na kuwauliza kwanini Radio na TV za
Tanzania haziwalipi wasanii pindi wanapoziga nyimbo zao kwenye vituo
vyao.
Professor
ameiambia Bongo5 kuwa baada ya kupeleka shauri hilo, wahusika ambao ni
COSOTA wamesema bado wapo kwenye vikao kujadili suala hilo.
“COSOTA
sio watu wa mwisho, wameniambia kuna vikao vingine vinaendelea, tuweke
subira lakini hili suala linajadiliwa kila siku. Budget ya serikali
imepita hakuna kilichoendelea, kama ni matatizo yapo kwenye sheria
kwanini isirekebishwe? Lakini tuseme kweli haya mambo yanatakiwa yaanze
ingawa kumekuwa na changamoto. Hata wasanii wenyewe wanafanya muziki
kama muziki ilimradi wanajifurahisha, lakini kama watakuwa serious
vyombo vya habari ‘Radio na TV’ kwa kuwalipa wasanii, maana yake hata
wasanii wenyewe watakuwa serious kufanya muziki kwa perfect na itachuja
upi mchele zipi pumba, naamini hivyo,” amesema.
“Vyombo
vya habari haviwezi kukubali kumlipa mtu ambaye yupo shaghalabaghala
ambao hawafanyi muziki ambao unaeleweka. Kenya wenzetu wanalipwa,
nimekuawa nikishauriana na wasanii wa Kenya kuhusu hili suala,
wakaniambia Kenya kuna baadhi ya wasanii ambao wapo kwenye COSOTA yao,
kwahiyo inakuwa ni rahisi wenyewe kuangalia ni jinsi gani wasanii wao
wananufaika na muziki wao. Kwetu hapa hili swala likipita kwanza wasanii
watanufaika na kazi zao pamoja na serikali itanufaika, pia Radio na TV
wakitaka wanufaike na muziki wa wasanii watadili na matangazo, sio kama
sasa hivi, TV na Radio zinaingiza pesa nyingi kwa matangazo kutokana na
kupiga nyimbo zao kwenye vipindi vyao,” aliongeza.
Professor amewataka wasanii wengine kuungana katika kulifuatilia suala hilo.
“Kinachoonekana
kwa wasanii wengi wa Bongo tunaogopa kumfunga Paka kengele, wengi
tunaogopa wakati muziki ndo wenye manufaa kwetu. Sasa hivi na baadaye,
wazee wetu akina mzee Marijani, Remmy Ongara mwenyezi Mungu amlaze
mahali pema, wao tayari wakati wao umepita, sasa hivi ni jukumu letu
kuutoa muziki hapa ulipo na kuupeleka kwenye next level na kuwafanya
watu wote waweze kunufaika kwa njia moja ama nyingine, ukiangalia kwenye
TV wana matangazo kibao hayo yote yapo kwa manufaa yao kwanini na
mwanamuziki asinufaike.”
0 comments:
Post a Comment