Dogo Janja
Na Dotto Kahindi-Thisday Magazine, Blog za mikoa
Mwezi
Juni mwaka huu umekuwa ni mwezi wa huzuni na furaha kwa nyota wa muziki
wa Bongo Fleva , Abdul Abubakar Chande ‘Dogo Janja’ kufuatia kutimuliwa
na Baba yake kimziki Madee na baada ya siku chache kurejea Dar es
Salaam na kuingia mkataba mpya na kampuni ya Mtanashati Entertainments.
Dogo
Janja alitimuliwa na Madee na kurejeshwa kwao jijini Arusha kwa madai
ya kushindwa kuzingatia masomo kwa kuendekeza utoro shuleni, kukosa
mwenendo mwema kimaadili sababu ambazo hata hivyo Dogo Janja
alizikanusha na kudai kuwa alikuwa akinyanyaswa na Madee.
Alidai
kuwa akiwa chini ya usimamizi wa Madee alikuwa akilipwa posho kidogo
baada ya kufanya maonyesho na kwamba Madee alihusika kumwibia pesa zake
benki hali iliyomfanya kuwa na salio la Tsh.25, 000 elfu tu katika
akaunti yake.
Hali
ilikuwa hivyo na imeleta picha mbaya na kuibua maswali mengi kwa
mashabiki wa muziki lakini lawama kubwa zinafaa kupelekwa kwa wazazi wa
Dogo Janja ambao walimruhusu kwa moyo mweupe aje kuishi na watu ambao
leo hii wanaonekana kuwa ni wahuni.
Pamoja
na kutimuliwa na Madee lakini sasa sasa amerejea tena akiwa katika
mwonekano mwingine, naamini muda mfupi aliokaa na wazazi wake walifanya
mazungumzo ya kutosha na kufanya makubaliano ya nini kipewe kipaumbela
katika maisha yake kwa sasa, ili kumjengea mafanikio yake kielimu na
kimaisha pia.
Furaha
aliyoipata baada ya kutua Bongo na kujiunga na kampuni ya Mtanashati
Entertainments ya jijini Dar es Salaam, zisimfanye akajisahau tena na
kuendeleza upuuzi alioufanya akiwa na Madee.
Tukubaliane
wote kuwa Dogo Janja bado ni mtoto na anahitaji kupata mwongozo wa
kutosha kutoka hasa kwa wazazi wake na watu walio juu ya uwezo wake ili
kumsaidia kufanya kila hatua kwa usahihi asije kujuta baadaye.
Pengine
kwa hatua ya nyota huyo cha kwenda kusomewa kisomo maalumu cha kuomba
Mwenyezi Mungu amnyooshee mambo yake pindi atakapoanza kushusha ngoma
mpya kinaweza kuonyesha kuwa kuna nia njema kwa watu alionao sasa.
Maneno
ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ostaz Juma na Musoma kuwa wameamua
kumfanyia kisomo hicho kwa lengo la kuweka kazi zote za Dogo janja
mikononi mwa Mungu ili kumkinga na watu wabaya ambao kwa namna moja ama
nyingine hawajafurahishwa na mpango mzima wa dogo huyo kurejea Bongo.
Hata
hivyo katika kipindi kifupi alichojiunga na kampuni hiyo Dogo janja
amefanyiwa ‘shopingi’ ya nguvu kwenye maduka makubwa ya viwalo yaliyopo
Mlimani City jijini Dar ambayo ilitumia zaidi ya shilingi Milioni 2.5.
Hivi
ni miongoni mwa vitu vinavyomfanya Dogo Janja afurahie kuwa katika
kampuni hiyo lakini lazima ajue kuwa nidhamu ya kazi ndiyo itamfanya
aendelee kupata matunda hayo maana akiendelea kujifanya nunda na kupuuza
ya wakubwa wake haitamsaidia.