Monday, July 16, 2012

SERENGETI, MIKUMI, MANYARA TUNASHINDWA NINI KUFANYA HAYA?



Barabara kuu ya Ecoduct De Woeste Hoeve A50, Netherlands; Nchi ya Netherlands inaidadi kubwa ya wanyama zaidi ya 600 ambao hutumia daraja hilo la aina yake kuvuka barabara.



HUU SI UHARIBIFU WA MAZINGIRA?

BREAKING Newzz>>>CHEGE apata ajali mbaya ya gari usiku huu Temeke


BREAKING: Msanii CHEGE apata ajali mbaya ya gari usiku huu Temeke Dar es salaam, ameumia ila gari halifai kabisa. Chanzo ni mtu wa pikipiki
Dj Sek

Saturday, July 14, 2012

Afande Sele azijibu shutuma za 20 Percent


Uswahiba kati ya wasanii wawili wa Bongo Flava nchini, Afande Sele na 20 Percent umeingia dosari baada ya kutupiana maneno kila mmoja kwa nyakati tofauti kwenye vyombo vya habari.

Maneno hayo yalianza wiki iliyopita baada ya Afande Sele kuzungumza na Clouds FM na kudai kusikitishwa na kitendo cha swahiba wake 20 Percent cha kugoma kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za Zanzibar wakati alikuwa amelipwa pesa zote.

Kufuatia mgomo huo, waandaaji walimpeleka lock-up msanii huyo na kubaki na laptop yake mpaka pale atakapowarudishia waandaji hao shilingi milioni moja waliyompa kwaajili ya kuperform kwenye tuzo hizo.

Hatimaye jana 20 Percent alizungumza na kituo hicho cha radio kuhusiana na tukio lenyewe na kusema kuwa Afande Sele amechanganyikiwa na anasumbuliwa na njaa ndio maana anamlaumu.

Akiongea kwa jaziba, 20 Percent amesema Afande Sele ni kama ‘mtoto’ na alimshangaa kufahamu kuwa alifika Zanzibar saa sita usiku bila kuwa sehemu ya kulala kutokana na waandaaji hao kuwa wababaishaji.

Leo (July 14) Afande Sele ametoa maelezo marefu kuhusiana na sakata hilo kupitia Facebook. Hivi ndivyo alivyoandika:

“Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twenty Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.

Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).

Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).

Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.

Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma "MBELE YAKO NYUMA YANGU" .. Kuna mstari Nilisema " ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugumu, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu".

Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.

Verry sorry kwa wote ambao mmefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.

Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

Chanzo: Leotainment blog

MAFANIKIO YA CHAMELEONE KATIKA MAISHA


.
Baada ya kukutana na staa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone nimegundua kuna mambo mengi nilikua nayasikia tofauti na kuyasoma ambayo yeye ameyazungumza tofauti kabisa.
Nilikua sijui, kumbe Chameleone alianza kuenjoy kuwa staa kuanzia mwaka 2000 japo alianza muziki 1995, 2003/2004 ndio alianza kupata pesa na hapo ndipo maajabu yalianza kutokea kwa kuanza kutimiza ndoto.



Jose Chameleone hapa akiwa  na Millard Ayo wa  Clouds
Chameleone amesema “nilijenga nyumba yangu kwa miaka miwili ambapo 2005 ilimalizika na ikawa imegharimu shilingi milioni 200 -300 za kitanzania, wakati nilikua naijenga hiyo ndio pesa niliyokua nayo na nikasema kabla sijaipoteza acha nifanye kitu muhimu lakini Mungu akanibariki tena baada ya kujenga hiyo nyumba nikapata bahati nyingine nikaendelea na vitu vingine”

Jose Chameleone (katikati) akiwa kwenye shooting ya moja ya video 

Exclusive na millardayo.com Mwimbaji huyu staa kutoka Uganda amesema vyanzo vyake vikubwa vya mapato kwa sasa ni kununua na kuuza ardhi, kuuza simu za mkononi ziitwazo Chameleone anazozitengeza China, kununua nyumba na kuziuza pia kupangisha nyumba.
kuhusu vyanzo vingine vya mapato Chameleone amesema “show pia zinatulipa sana Uganda japo siwezi kukwambia nalipwa bei gani kwa sababu sipendi kuonekana mtu wa kujisifia lakini kwa wiki moja naweza kupiga show mbili Kampala au Uganda, na kingine kinachotulipa sana ni Kampuni kubwa za biashara ambazo zikikuona una nguvu zinakuchukua na kukulipa vizuri kwa kufanya nao promoshen au mambo mengine ya mkataba wa biashara”



Hii ni kwa  Hissani ya  www.millardayo.com

Friday, July 13, 2012

MAFUNZO YA MUZIKI 2012


Tuesday, July 3, 2012

MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI

ACTION MUSIC TANZANIA (AMTZ) YENYE NAMBA YA USAJILI BST/4733 ITATOA MAFUNZO YA UPIGAJI WA ALA MBALIMBALI ZA MUZIKI (KWA VITENDO) KWA WATU WOTE

MAFUNZO YATAANZA: TAREHE 16/07/2012

MAHALI: IDARA YA SANAA NA SANAA ZA MAONESHO (FPA) CHUO
                     KIKUU CHA DAR ES SALAAM (SEHEMU YA MLIMANI)

NJOO UJIFUNZE MBINU ZA KITAALAMU ZA KUPIGA/KUCHEZA  GITAA, KEYBOARD/PIANO, TARUMBETA, SAXOPHONE, KONGA, DRUM SET, NA UPIGAJI WA NGOMA ZA ASILI YA TANZANIA, BILA KUSAHAU MAFUNZO MAALUMU YA “BODY PERCUSSION” (Matumizi ya mwili kutengeneza midundo ya muziki) NA USOMAJI WA “NOTATION” YATAKAOTOLEWA NA WATAALAM WALIOBOBEA KATIKA TASNIA YA MUZIKI KUTOKA VYUO MBALIMBALI.

USAJILI UNAFANYIKA: IDARA YA SANAA NA SANAA ZA MAONESHO (FPA) CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (MLIMANI)
FOMU ZA USAJILI ZINAPATIKANA FPA SAA 4:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI KWA GHARAMA YA SHILINGI 3000/= TU. WAHI, NAFASI NI CHACHE.

KWA MAWASILIANO:  +255 757 361 266
                                                +255 714 553 239
                                                +255 755 058 045
E-mail: actionmusictz@yahoo.com/mandolintz@yahoo.co.uk/mpepodamas@gmail.com
www.actionmusictz.blogspot.com

NYOTE MNAKARIBISHWA