Friday, March 25, 2011

CHOMBO CHA MUZIKI KINAPIGA CHOMBO CHA MUZIKI

Mandoli Kahindi, akionyesha namna ya kupiga kinanda

TUNAJIPANGA ZAIDI

Kauzeni Lyamba, mpaka chee, akionyesha makeke yake katika kinanda

NI KAZI KWENDA MBELE

Edwin Mwakibete, AMTZ

LIMEKAA VYEMA TWENDE KAZI

Mwalimu Lazaro Kayombo akitune vyema gita

NINACHECK NA KUREKEBISHA

Mwalimu wa muziki wa AMTZ Geofrey Charahan akifunga konga tayari kwa workshop ya siku tatu UDSM

SIKU YA KWANZA, AMTZ WAKUTANA UDSM

Maandalizi ya kazi ya mwishoni mwa wiki, vyombo viko safiii

Wednesday, March 23, 2011

AMTZ KUKUTANA WEEKEND HII

Na Dotto Kahindi
Walimu wa muziki Tanzania kutoka shirika la Action Music Tanzania wanakutana ijumaa hii katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa mafunzo ya muziki yatakayodumu kwa siku tatu.
Pamoja na mambo mengine walimu hao watajifua njia sahihi za kufundishia namna ya kuandika na kusoma muziki, mazoezi ya mnyumbuliko wa mwili na hamoni.

Tuesday, March 15, 2011


Vijana wa kazi, wakionyesha namna ya kuzicharaza ngozi

Monday, March 7, 2011

                                         Body Purcussion inafanya kazi hapo, kazi kwelikweli

Saturday, February 26, 2011

GMA

Where real musicians belongs

Maunda Zoro kumiliki Bendi Tanzania



MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Maunda Zoro asema hivi karibuni ataanzisha Bendi yake mwenyewe. Akizungumza na Mwananchi Jumapili hivi karibuni, Maunda alisema;  “Wazo la kuanzisha bendi nilipewa na kaka (Banana Zoro), lakini taratibu za kuanzisha bendi hiyo bado kidogo kukamilika. Alisema kuna baadhi ya vifaa havijakamilika, lakini anategemea hadi Aprili mwaka huu atakuwa tayari ameshaianzisha ikiwamo kusajili bendi hiyo. “Jina la bendi bado sijalifikiria, ingawa nitawashirikisha baadhi ya wanamuziki wa Bongo fleva ambao sitawataja majina kwa sasa, kwani ni mapema mno,” alisema Maunda. Maunda alitamba na wimbo wa ‘Niwe wako’ na ‘Mapenzi ni ya wawili’ na ameshirikishwa kwenye nyimbo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hellow wa Hussein Machozi na ‘Usinihukumu’ wa  Steve.


Mwalimu wa muziki Geofray Charahani wa AMTZ akicheza Violin