Saturday, November 17, 2012

Alliance Francois na onesho la utamaduni

na Khadija Kalili.
KITUO cha Utamaduni cha Ufaransa ‘Alliance Francois’ kimeandaa onesho la bure la muziki wa utamaduni wa Mwafrika katika kituo chake kilichoko Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es Salaam leo jioni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa kituo hicho, Michael Shuma, aliwataja wasanii watakaonogesha onesho la leo kuwa ni Maryse Ngalula kutoka Kinshansa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Elie Kamano ‘General Kamano’ wa Guinea, ambaye anapiga muziki wake katika miondoko ya Hip Hop.
Alisema katika tamasha hilo, wasanii hao wawili watatumbuiza mmoja mmoja na baadaye watatoa burudani kwa pamoja.
Koshuma aliongeza kwamba, kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kufanya maonesho ya utamaduni mara kwa mara, na wanawashukuru wadhamini wao Shirika la Ndege la Precision kwa kutoa usafiri kwa wasanii hao, ambao mara baada ya onesho la Dar es Salaam watakwenda Arusha Jumapili, kisha Kilwa ambako nako watafanya maonesho.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment