Wandaaji wa tamasha la kila mwaka la Sauti za Busara, Busara Promotions wameandaa shindano la uandishi wa makala mbalimbali kuhusiana na tamasha hilo zitakazochapishwa mtandaoni na kwenye magazeti na washindi kuzawadiwa zawadi mbalimbali.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, Busara Promotions imeandika:
Hii ni stori kwa ajili ya waandishi, wachapishaji na wenye mitandao ya kijamii. Kitu pekee katika tamasha la kumi la Sauti za Busara ambalo litaanza tarehe 14- 17 Februari 2013. Tamasha limefikia muongo mmoja ambalo hakuna mfano wake. Waandishi wanaombwa kutuma makala mitandaoni, blog na wachapishaji wa magazeti.
Mbali na kushapisha na kuweka makala mbalimbali, makala bora na mwandishi/mtunzi bora atazawadiwa fulana ya tamasha, pasi ya bure ya siku zote za tamasha na Posho kama ishara ya shukrani. Tuma kupitia barua pepe hii press@busara.or.tz mwisho tarehe 30/11/2012.
Tunasubiria kupokea makala bora. Tutawapa idhini waandishi bora kuendelea kuweka makala zao, chapisho mbalimbali kwenye blogs na tovuti baada ya tarehe ya mwisho. Makala bora itajadiliwa kutokana na uhalisia, mtazamo na idadi ya mitazamo/maoni kutoka kwa wasomaji na mashabiki.
Kuhusu Sauti za Busara
Sauti za Busara hufanyika kila mwezi wa pili katika kisiwa cha marashi ya karafuu Zanzibar, tamasha hujulikana kama ‘Tamasha rafiki katika sayari ya Dunia’. Katika kuwawezesha wenyeji ili wafurahie tamasha bei ya tiketi kwa kila siku ni shilingi 3,000 kwa watanzania na wageni kutoka nchi za nje ni Dola 48 za kimarekani.
Tamasha la 10 litakutanisha vikundi mbalimbali kama ifuatavyo Cheikh Lô (Senegal) Mlimani Park Orchestra (Tanzania) Khaira Arby (Mali) Comrade Fatso and Chabvondoka (Zimbabwe) Culture Musical Club (Zanzibar / Tanzania) Atongo Zimba (Ghana / UK) N’Faly Kouyaté (Guinea) Nathalie Natiembe (Reunion) Zanzibar Unyago (Zanzibar / Tanzania) Nawal & Les Femmes de la Lune (Comoros / Mayotte) Wazimbo (Mozambique) The Moreira Project (Mozambique / South Africa) Owiny Sigoma Band (Kenya / UK) Mokoomba (Zimbabwe) Msafiri Zawose & Sauti Band (Tanzania) Mani Martin (Rwanda) Burkina Electric (Burkina Faso / USA) Lumumba Theatre Group(Tanzania) Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden) Super Maya Baikoko (Tanzania) Peter Msechu (Tanzania) Wakwetu Jazz Vibes (Tanzania) Safi Theatre Group (Tanzania) na wengineo.
Sauti za Busara hufanikiwa kuwaleta wageni wengi kila mwaka, lakini huifadhi misingi ya wenyeji. Hutoa fursa kwa wenyeji kuona na kusikiliza muziki kutoka sehemu mbalimbali za Afrika na vilevile kuutambulisha muziki wa Afrika Mashariki kwa wageni, fursa hii ni adhimu sana kiafya na kimaendeleo ya kimuziki.
Tamasha huwakutanisha watu pamoja kusheherekea na umoja, bila ya kuzingatia itikadi zao za kisiasa na kidini. Fursa kama hii ni adimu sana Zanzibar, na tukio hili limekuwa ni kiungo na muhimu katika kuimarisha umoja na amani, kujenga mahusiano mema na kuheshimiana.
Zaidi ya hayo, siku hizi watu wengi hutafuta mbinu muafaka za kujiwezesha kiuchumi kila, kupitia muziki na sanaa mbalimbali. Kwa matarajio yetu makubwa kabisa kwamba wageni huja kwa wingi na hutegemea kupata vitu adhimu kabisa kutoka kwetu, kama kufurahia muziki wakiwa na wenyeji wao.
Tamasha husaidia ukuwaji wa kiuchumi. Takwimu ya Serikali imeonyesha idadi ya wageni wanaokuja Zanzibar imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 500 tangu lilipoanza tamasha.
Tamasha la Sauti za Busara hutoa mfano wa tukio ambalo lenye muundo wa kimaendeleo kwa pande zote wageni na wenyeji, kwa uthamini utajiri wa tamaduni mbalimbali za kiafrika. Huonyesha uzuri wa muziki wa tamaduni za kiafrika, na uwezekano wa kutengeneza ajira na kujiongezea kipato.
0 comments:
Post a Comment