Monday, December 16, 2013

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI

Action Music Tanzania (AMTZ) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza desemba 19 mwaka huu, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu na magorofa ya jeshi ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828 au barua pepe, actionmusictz@yahoo.com, Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org
 Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
 Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho

Thursday, December 12, 2013

Arts and culture contribute more to U.S. economy than tourism

For the first time the federal government has tallied up the arts and culture contribution to the nation’s economy. It turns out that sector, movies, painting, publishing, cable and more, was worth half a trillion dollars -- 3 percent to the gross domestic product in 2011. That’s more than the travel and tourism industry.
“Here you have for the first time, comprehensive empirical evidence from the point of view of economists that the arts play a substantial role in the nation’s economy,” says Sunil Iyengar who runs the Office of Research and Analysis for the National Endowment for the Arts.
In an instant, writers, app designers, publishers and painters just got a bunch of "street cred." Nearly two million people work in the arts and culture industry which exported about $40 billion in goods and services in 2011. Some economists say ideas, innovation, and creativity are essential to growing the United States economy.
University of Minnesota culture economist Ann Markusen says putting a dollar value to the sector could lead to policies that promote it. “The recognition of the significance of art skills, is going to really be a big boost for artists and also for encouraging young people to go into the arts,” she says.
Who knows, maybe that whole starving artist thing will finally be on its way out.

Tuesday, December 10, 2013

TANGAZO: WANATAFUTWA WAIMBAJI CHIPUKIZU WA MUZIKI WA UNJILI

HABARI   NJEMA   KWA   WAIMBAJI  CHIPUKIZI  WA  MUZIKI   WA    INJILI  TANZANIA.

Wewe ni  kijana  wa  kikristo  uliye  okoka ?
Una  karama  ya  uimbaji ?
Unataka  kumtumikia  na  kumtangaza  Mungu  kwa  njia  ya  uimbaji  ?
Kama  jibu  ni  ndio  basi  hii  ni  habari  njema  sana  kwako.
Huduma  Ya  UPENDO  & FURAHA  ya  jijini  Dar  Es  salaam, inatafuta  vijana  wa  kikristo    walio  okoka, kwa  ajili   ya  kuanzisha  huduma ya  muziki  wa  injili  itakayo  kuwa  ikihudumu  katika  mikoa mbalimbali  ya Tanzania  na  katika  nchi  jirani.
SIFA   ZA   WATU   WANAO   HITAJIKA  :
i.             Awe  na  karama  ya  uimbaji
ii.            Awe  na  Umri   wa   kuanzia  miaka  16  hadi  35.
iii.          Awe  ameokoka  na  mwenye  hofu  kuu  ya  Mungu.
iv.           Awe  na  wito  wa  kweli   wa  kumtangaza  na  kumtumikia  Mungu  kwa  njia  ya  uimbaji.
v.             Awe  na  utayari , pamoja  na   muda  wa  kutosha   wa  kusafiri  na  huduma  katika  mikoa mbalimbali  ya  Tanzania  pamoja  na  nchi  jirani.
vi.           Awe  mkazi  wa  Dar  Es  salaam .

USAILI  utafanyika  siku  ya  tarehe  06  January  2013.
MWISHO  wa  kujiandikisha  ni  tarehe  24  Desemba  2013.
Kujiandikisha,  fika  moja  kwa  moja  ofisini  kwetu, siku za  kazi kuanzia  saa  tatu kamili  asubuhi  hadi  saa kumi  kamili  jioni, au   wasiliana  nasi  kwa   SIMU   0784406508

Thursday, June 27, 2013

British Council yatoa mafunzo ya uongozi na biashara kwa viongozi wa taasisi za sanaa na sanaa za maonesho

 Washiriki katika mafunzo ya uongozi na biashara yananofanyika kwenye Ukumbi wa Nafasi Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo hayo, washiriki hao wametoka katika taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na sanaa na sanaa za maonesho.



Mafunzo haya yanatolewa na Britishi Council, na mwezeshaji ni Faisal Kiwewa kutoka shirika la Bayimba la nchini Uganda.

Tuesday, May 14, 2013

GOETHE INSTITUT-TANZANIA INVITE YOU TO AN OPEN STAGE NIGHT




On our OPEN STAGE NIGHT we invite you to perform. Whatever your talents might be, everyone is welcome to show them on stage. Please register now by sending us an e-mail or call us.E-mail: intern@daressalaam.goethe.org, Tel.:  075 375 152 and Tell us what you are planning to perform and the required technical equipment. 

Musicians can also bring their own instruments. entrance is fees.




Monday, May 13, 2013

USAJILI WA TUZO ZA MUZIKI ZA RFI WAANZA, WANAMUZIKI TANZANIA CHANGAMKIENI FURSA HII


Kwa usajili wa tuzo za muziki za rfi ambazo hufanyika kila mwaka na kuwashirikisha wanamuziki mbalimbali katika bara la Afrika bonyeza hapo chini rfi music award registration

Friday, May 10, 2013

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA SEMINA YA SOKO LA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI 'DOADOA' JINJA UGANDA


 Washiriki katika semina ya kujadili changamoto za soko la muziki Afrika Mashariki wakifuatilia moja ya mada kwenye hotel ya Crasted Crane mjini Jinja, Uganda
 Mwanmuziki kutoka Kenya, Winyo akitumbuiza katika moja ya matamasha yanayoambatana na semina ya kujadili changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki.
 Wanamuziki wakiimba wimbo wa ushirikiano katika moja ya matamasha yanayoambatana na semina ya kujadili changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki, kutoka kushoto ni Mani Martin kutoka Rwanda, Shamsila kutoka Arusha Tanzania na Staffi kutoka Uingereza.


Kwa picha za matukio zaidi tembelea DOADOA 2013

Wednesday, May 8, 2013

SEMINA YA KUJADILI CHANGAMOTO ZA SOKO LA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI 'DOADOA' YAFANYIKA UGANDA

Waendesha mada katika semina ya kuangalia changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki na njia za kuzitatua wakijadili umuhimu wa elimu ya muziki katika soko la muziki, kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Action Music Tanzania, Mandoli Kahindi, Mkurugenzi wa sanaa kutoka Global Music Academy Ujerumani,William Ramsay, Muaandaaji wa muziki wa Uganda, Kazi Kasozi na Mkurugenzi Mtendaji wa Ketebul Music Kenya, Tabu Osusa


Semina hiyo ambayo inaambatana na maonyesho ya kazi mbalimbali za muziki yameandaliwa na Bayimba Cultural Foundation ya Uganda ambapo wadau mbalimbali wa muziki kutoka nchi mbalimbali wamejumuika kujadili na kubadilishana uzeofu juu ya soko la muziki kwa nchi za Afrika Mashariki. picha za matukio zaidi tembelea DOADOA