Action Music Tanzania (AMTZ) inatangaza
fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza
desemba 19 mwaka huu, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala
na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na
upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga,
drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body
percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye
ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu na magorofa ya jeshi ambapo ili
kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828 au barua pepe,
actionmusictz@yahoo.com,
Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org
Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho
0 comments:
Post a Comment