HABARI NJEMA KWA WAIMBAJI CHIPUKIZI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.
Wewe ni kijana wa kikristo uliye okoka ?
Una karama ya uimbaji ?
Unataka kumtumikia na kumtangaza Mungu kwa njia ya uimbaji ?
Kama jibu ni ndio basi hii ni habari njema sana kwako.
Huduma Ya UPENDO & FURAHA ya jijini Dar Es salaam, inatafuta vijana wa kikristo walio okoka, kwa ajili ya kuanzisha huduma ya muziki wa injili itakayo kuwa ikihudumu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na katika nchi jirani.
SIFA ZA WATU WANAO HITAJIKA :
i. Awe na karama ya uimbaji
ii. Awe na Umri wa kuanzia miaka 16 hadi 35.
iii. Awe ameokoka na mwenye hofu kuu ya Mungu.
iv. Awe na wito wa kweli wa kumtangaza na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
v. Awe na utayari , pamoja na muda wa kutosha wa kusafiri na huduma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi jirani.
vi. Awe mkazi wa Dar Es salaam .
USAILI utafanyika siku ya tarehe 06 January 2013.
MWISHO wa kujiandikisha ni tarehe 24 Desemba 2013.
Kujiandikisha, fika moja kwa moja ofisini kwetu, siku za kazi kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni, au wasiliana nasi kwa SIMU 0784406508
0 comments:
Post a Comment