Action
Music Tanzania inayofuraha ya kukualika kuhudhuria onesho la muziki
litakalofanyika siku ya Ijumaa ya tarehe saba mwezi wa tatu (07.03.2014)
kwenye idara ya sanaa na sanaa za maonesho (FPA) Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam kuanzia saa kumi na mbili na nusu jioni hadi saa mbili usiku
(12:30-2:00), Kiingilio ni bure.
Onesho
hilo limeandaliwa na AMTZ litawahusisha wanamuziki kutoka kwenye
taasisi mbalimbali ambao wameshiriki mafunzo maalumu ya muziki kwa muda
wa wiki mbili ambayo yamefanyika kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za
Maonesho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (FPA), kuanzia Februari 24
mwaka huu. Pia wakati wa onesho kutakuwa na zoezi la kuchangia mfuko wa
AMTZ ambapo wageni wataombwa kuchangia kiasi chochote cha fedha ili
kuijengea uwezo asasi wa kuendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo kwa watu
wengine.
AMTZ
ni asasi isiyo ya kiserikali inayoundwa na walimu wa muziki kutoka
katika taasisi mbalimbali za elimu ya muziki nchini na imesajiliwa na
BASATA na kupata kibali cha kutoa mafunzo ya muziki ya muda mfupi. AMTZ
imekuwa ikitoa mafunzo ya muziki kwa wanamuziki wa aina zote kwa lengo
la kuwajengea uwezo wa kuandaa, kucheza na kufundisha muziki kwa kutumia
mbinu mpya na za kitaalamu ili kuambukiza elimu ya muziki kwa
wanamuziki wengine na hatimaye kuboresha ustawi wa muziki kwa ujumla
wake nchini.
Kufika
kwako katika onesho hilo utakuwa ni mchango mkubwa sana kwa wanamuziki
wetu, asasi yetu na muziki kwa ujumla wake. Natanguliza shukran zangu za
dhati na karibu sana
Contact:
Mandolin Kahindi
Executive Secretary
Action Music Tanzania
0 comments:
Post a Comment