Saturday, July 14, 2012

MAFANIKIO YA CHAMELEONE KATIKA MAISHA


.
Baada ya kukutana na staa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone nimegundua kuna mambo mengi nilikua nayasikia tofauti na kuyasoma ambayo yeye ameyazungumza tofauti kabisa.
Nilikua sijui, kumbe Chameleone alianza kuenjoy kuwa staa kuanzia mwaka 2000 japo alianza muziki 1995, 2003/2004 ndio alianza kupata pesa na hapo ndipo maajabu yalianza kutokea kwa kuanza kutimiza ndoto.



Jose Chameleone hapa akiwa  na Millard Ayo wa  Clouds
Chameleone amesema “nilijenga nyumba yangu kwa miaka miwili ambapo 2005 ilimalizika na ikawa imegharimu shilingi milioni 200 -300 za kitanzania, wakati nilikua naijenga hiyo ndio pesa niliyokua nayo na nikasema kabla sijaipoteza acha nifanye kitu muhimu lakini Mungu akanibariki tena baada ya kujenga hiyo nyumba nikapata bahati nyingine nikaendelea na vitu vingine”

Jose Chameleone (katikati) akiwa kwenye shooting ya moja ya video 

Exclusive na millardayo.com Mwimbaji huyu staa kutoka Uganda amesema vyanzo vyake vikubwa vya mapato kwa sasa ni kununua na kuuza ardhi, kuuza simu za mkononi ziitwazo Chameleone anazozitengeza China, kununua nyumba na kuziuza pia kupangisha nyumba.
kuhusu vyanzo vingine vya mapato Chameleone amesema “show pia zinatulipa sana Uganda japo siwezi kukwambia nalipwa bei gani kwa sababu sipendi kuonekana mtu wa kujisifia lakini kwa wiki moja naweza kupiga show mbili Kampala au Uganda, na kingine kinachotulipa sana ni Kampuni kubwa za biashara ambazo zikikuona una nguvu zinakuchukua na kukulipa vizuri kwa kufanya nao promoshen au mambo mengine ya mkataba wa biashara”



Hii ni kwa  Hissani ya  www.millardayo.com

Friday, July 13, 2012

MAFUNZO YA MUZIKI 2012


Tuesday, July 3, 2012

MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI

ACTION MUSIC TANZANIA (AMTZ) YENYE NAMBA YA USAJILI BST/4733 ITATOA MAFUNZO YA UPIGAJI WA ALA MBALIMBALI ZA MUZIKI (KWA VITENDO) KWA WATU WOTE

MAFUNZO YATAANZA: TAREHE 16/07/2012

MAHALI: IDARA YA SANAA NA SANAA ZA MAONESHO (FPA) CHUO
                     KIKUU CHA DAR ES SALAAM (SEHEMU YA MLIMANI)

NJOO UJIFUNZE MBINU ZA KITAALAMU ZA KUPIGA/KUCHEZA  GITAA, KEYBOARD/PIANO, TARUMBETA, SAXOPHONE, KONGA, DRUM SET, NA UPIGAJI WA NGOMA ZA ASILI YA TANZANIA, BILA KUSAHAU MAFUNZO MAALUMU YA “BODY PERCUSSION” (Matumizi ya mwili kutengeneza midundo ya muziki) NA USOMAJI WA “NOTATION” YATAKAOTOLEWA NA WATAALAM WALIOBOBEA KATIKA TASNIA YA MUZIKI KUTOKA VYUO MBALIMBALI.

USAJILI UNAFANYIKA: IDARA YA SANAA NA SANAA ZA MAONESHO (FPA) CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (MLIMANI)
FOMU ZA USAJILI ZINAPATIKANA FPA SAA 4:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI KWA GHARAMA YA SHILINGI 3000/= TU. WAHI, NAFASI NI CHACHE.

KWA MAWASILIANO:  +255 757 361 266
                                                +255 714 553 239
                                                +255 755 058 045
E-mail: actionmusictz@yahoo.com/mandolintz@yahoo.co.uk/mpepodamas@gmail.com
www.actionmusictz.blogspot.com

NYOTE MNAKARIBISHWA

Saturday, June 30, 2012

Exclusive uchambuzi: Wazazi wa Dogo Janja fuatilieni maendeleo yake, msiwaachie Mapromota

Dogo Janja
Na Dotto Kahindi-Thisday Magazine, Blog za mikoa

Mwezi Juni mwaka huu umekuwa ni mwezi wa huzuni na furaha kwa nyota wa muziki wa Bongo Fleva , Abdul Abubakar Chande ‘Dogo Janja’ kufuatia kutimuliwa na Baba yake kimziki Madee na baada ya siku chache kurejea Dar es Salaam na kuingia mkataba mpya na kampuni ya Mtanashati Entertainments.
Dogo Janja alitimuliwa na Madee na kurejeshwa kwao jijini Arusha kwa madai ya kushindwa kuzingatia masomo kwa kuendekeza utoro shuleni, kukosa mwenendo mwema kimaadili sababu ambazo hata hivyo Dogo Janja alizikanusha na kudai kuwa alikuwa akinyanyaswa na Madee.
Alidai kuwa akiwa chini ya usimamizi wa Madee alikuwa akilipwa posho kidogo baada ya kufanya maonyesho na kwamba Madee alihusika kumwibia pesa zake benki hali iliyomfanya kuwa na salio la Tsh.25, 000 elfu tu katika akaunti yake.
Hali ilikuwa hivyo na imeleta picha mbaya na kuibua maswali mengi kwa mashabiki wa muziki lakini lawama kubwa zinafaa kupelekwa kwa wazazi wa Dogo Janja ambao walimruhusu kwa moyo mweupe aje kuishi na watu ambao leo hii wanaonekana kuwa ni wahuni.
Pamoja na kutimuliwa na Madee lakini sasa sasa amerejea tena akiwa katika mwonekano mwingine, naamini muda mfupi aliokaa na wazazi wake walifanya mazungumzo ya kutosha na kufanya makubaliano ya nini kipewe kipaumbela katika maisha yake kwa sasa, ili kumjengea mafanikio yake kielimu na kimaisha pia.
Furaha aliyoipata baada ya kutua Bongo na kujiunga na kampuni ya Mtanashati Entertainments ya jijini Dar es Salaam, zisimfanye akajisahau tena na kuendeleza upuuzi alioufanya akiwa na Madee.
Tukubaliane wote kuwa Dogo Janja bado ni mtoto na anahitaji kupata mwongozo wa kutosha kutoka hasa kwa wazazi wake na watu walio juu ya uwezo wake ili kumsaidia kufanya kila hatua kwa usahihi asije kujuta baadaye.
Pengine kwa hatua ya nyota huyo cha kwenda kusomewa kisomo maalumu cha kuomba Mwenyezi Mungu amnyooshee mambo yake pindi atakapoanza kushusha ngoma mpya kinaweza kuonyesha kuwa kuna nia njema kwa watu alionao sasa.
Maneno ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ostaz Juma na Musoma kuwa wameamua kumfanyia kisomo hicho kwa lengo la kuweka kazi zote za Dogo janja mikononi mwa Mungu ili kumkinga na watu wabaya ambao kwa namna moja ama nyingine hawajafurahishwa na mpango mzima wa dogo huyo kurejea Bongo.
Hata hivyo katika kipindi kifupi alichojiunga na kampuni hiyo Dogo janja amefanyiwa ‘shopingi’ ya nguvu kwenye maduka makubwa ya viwalo yaliyopo Mlimani City jijini Dar ambayo ilitumia zaidi ya shilingi Milioni 2.5.
Hivi ni miongoni mwa vitu vinavyomfanya Dogo Janja afurahie kuwa katika kampuni hiyo lakini lazima ajue kuwa nidhamu ya kazi ndiyo itamfanya aendelee kupata matunda hayo maana akiendelea kujifanya nunda na kupuuza ya wakubwa wake haitamsaidia.

Monday, February 27, 2012

2012 with new talents



Friday, December 23, 2011

TANGAZO! TANGAZO! TANGAZO!

ASASI YA ACTION MUSIC TANZANIA (AMTZ) YENYE NAMBA YA USAJILI BST/4733 IMEANDAA NA ITAENDESHA MAFUNZO YA MUZIKI (NADHARIA NA VITENDO) KWA WATU WOTE KUANZIA TAREHE 09/01/2012 IDARA YA SANAA NA SANAA ZA MAONESHO (FPA) CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

USAJILI UNAFANYIKA KATIKA OFISI ZETU (AMTZ) ZILIZOPO SHULE YA MSINGI MWENGE KARIBU NA MARYLAND BAR, KILA SIKU KUANZIA 20/12/2011 HADI 7/1/2012, SAA 4:00 HADI SAA 7:00 MCHANA, NA SAA 8:00 HADI SAA 11:00 JIONI. FOMU ZA USAJILI ZINAPATIKANA OFISINI KWA GHARAMA YA SHILINGI 3000/= TU

MAFUNZO YATAKAYOTOLEWA NI PAMOJA NA NADHARIA YA MUZIKI, UCHEZAJI/UPIGAJI WA ALA ZA MUZIKI ZIKIWEMO GITAA, KEYBOARD/PIANO, TARUMBETA, SAXOPHONE, KONGA, DRUM SET, NA UPIGAJI WA NGOMA ZA ASILI YA TANZANIA.

PIA YATATOLEWA MAFUNZO YA “BODY PERCUSSION” (Matumizi ya mwili kutengeneza midundo ya muziki)

KWA MAWASILIANO:-
                        +255 757 361 266
                        +255 716 515 853
                        +255 755 058 045
E-MAIL: actionmusictz@yahoo.com
www.actionmusictz.blogspot.com
 


Wednesday, September 21, 2011

MAFUNZO YA MUZIKI AGOSTI 2011, FPA, UDSM

Mwalimu wa muziki wa AMTZ Abeid Mussa akitoa maelekezo wakati mafunzo upande wa 'Music Ensemble'

Washiriki wa mafunzo ya muziki yaliyofanyika Agosti 8-21, 2011 wakifanya onyesho, katika kituo cha utamaduni cha Ujerumani, Goethe Institut-Tanzania kilichopo Upanga, Dar es Salaam

Thursday, August 18, 2011

Invitation to a Concert
Saturday 20.08. 2011, Time: 19:30 - 20:40, Venue: Goethe-Institut
Action Music Tanzania Concert
Action Music Tanzania has organized a concert to show the results of 14 days
 music training for budding musician from Dar es Salaam, Pwani and Shinyanga.
The participants of the music training will perform a Nyamwezi melody,
a Makonde melody and a body percussion.

Goethe-Institut Tanzania



Alykhan Road No. 63

Time: 19.30 - 20.40

Date: 20.08.2011


Music Training, at FPA,UDSM








Wednesday, August 10, 2011

MAFUNZO YA MUZIKI 10/08/2011

Mwalimu Geofrey Charahani akitoa maelekezo ya namna ya upigaji sahihi na wa kitaalamu wa vyombo vya kupiga (percussive instruments), Six ni miongoni mwa wanafunzi wanaoshiriki mafunzo ya muziki Agosti mwaka 2011.


Mwalimu Abeid Mussa na mwanafunzi wake wa gita




Mwalimu Damas Mpepo akitoa maelekezo kwa mwanafunzi wake wa chombo cha kupuliza mbinu muhimu katika kutumia chombo hicho.


Kwa mara ya kwanza Ishara ama Six akipiga drum baada ya kupewa maelekezo na mwalimu wake Geoffrey Charahani


Viongozi na walimu wa AMTZ wakiwa katika picha na baadhi ya wanafunzi wa mafunzo ya muziki


Viongozi na walimu wa AMTZ, waliosimama kutoka kulia ni Mratibu Damas Mpepo, Joyce Kirio, Katibu Mtendaji Mandolin Kahindi, Mweka Hazina Abeid Mussa, Mratibu Msaidizi Lazaro Kayombo, Suleiman Makame, Kauzeni Lyamba na Geoffrey Charahan, waliokaa ni baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzo ya muziki.

MAFUNZO YA MUZIKI

Friday, March 25, 2011

CHOMBO CHA MUZIKI KINAPIGA CHOMBO CHA MUZIKI

Mandoli Kahindi, akionyesha namna ya kupiga kinanda

TUNAJIPANGA ZAIDI

Kauzeni Lyamba, mpaka chee, akionyesha makeke yake katika kinanda

NI KAZI KWENDA MBELE

Edwin Mwakibete, AMTZ

LIMEKAA VYEMA TWENDE KAZI

Mwalimu Lazaro Kayombo akitune vyema gita

NINACHECK NA KUREKEBISHA

Mwalimu wa muziki wa AMTZ Geofrey Charahan akifunga konga tayari kwa workshop ya siku tatu UDSM

SIKU YA KWANZA, AMTZ WAKUTANA UDSM

Maandalizi ya kazi ya mwishoni mwa wiki, vyombo viko safiii

Wednesday, March 23, 2011

AMTZ KUKUTANA WEEKEND HII

Na Dotto Kahindi
Walimu wa muziki Tanzania kutoka shirika la Action Music Tanzania wanakutana ijumaa hii katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa mafunzo ya muziki yatakayodumu kwa siku tatu.
Pamoja na mambo mengine walimu hao watajifua njia sahihi za kufundishia namna ya kuandika na kusoma muziki, mazoezi ya mnyumbuliko wa mwili na hamoni.

Tuesday, March 15, 2011


Vijana wa kazi, wakionyesha namna ya kuzicharaza ngozi

Monday, March 7, 2011

                                         Body Purcussion inafanya kazi hapo, kazi kwelikweli